Bei Za Vitu Kupanda Sokoni Kariakoo

WAFANYABIASHARA wa Soko Kuu la Kariakoo wamewataka wateja wanaotumia soko hilo kutoshitushwa na bei mpya za bidhaa zitakazoanza kupanda kuanzia wiki ijayo.

WAFANYABIASHARA wa Soko Kuu la Kariakoo wamewataka wateja wanaotumia soko hilo kutoshitushwa na bei mpya za bidhaa zitakazoanza kupanda kuanzia wiki ijayo.
Wakizungumza na Mwananchi wafanyabiashara hao walisema kuanzia wiki ijayo hadi Januari, bei za bidhaa zitakuwa juu sana kutokana na kipindi hicho kuwa msimu wa siku kuu.
Hassan Hassan, mfanyabiashara kwenye soko hilo, alisema miezi ya Novemba na Desemba ni kipindi kilicho na sikukuu nyingi, hasa za Krismasi na Mwaka Mpya, hivyo bei za baadhi ya bidhaa lazima zitakuwa juu tofauti na miezi mingine.
Alisema: “Hivi sasa kuna siku kuu za ubarikio, Krismasi na mwaka mpya. Watu wanaanza kufanya maandalizi ndio maana tumeanza kuwaambia mapema kuwa bei zitabadilika kuanzia wiki ijayo, yaani bei zitakuwa hazishikiki hapa sakoni.”
Bidhaa ambazo mara nyingi hupanda bei katika kipindi hiki ni zile za watoto kama viatu, nguo na mapambo ya aina zote.
“Viatu vya watoto, hasa vya rangi nyeupe na nyeusi, nguo za ubarikio, viatu na nguo za watu wazima, vyote vitapanda sana bei kwa kuwa tunaangalia vitu vinavyoitajika sana miezi hii,” alisema mfanyabiashara wa nguo aliyejitambulisha kwa jina la Aziza.
Wafanyabiashara hao walisema kuwa hiyo miezi ndiyo ya kupata faida kwa kipindi kifupi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents