Habari

Bendi ya Marekani yaleta balaa Dar

Native DeenJumuiya na taasisi za kiislamu, zimeutaka Ubalozi wa Marekani nchini kuzuia tamasha la bendi ya Native Deen kwa hoja kuwa, wanamuziki wa bendi hiyo, wanakiuka madili ya Kiislamu.

Native Deen


JUMUIYA na taasisi za kiislamu, zimeutaka Ubalozi wa Marekani nchini kuzuia tamasha la bendi ya Native Deen kwa hoja kuwa, wanamuziki wa bendi hiyo, wanakiuka madili ya Kiislamu. Kwa mujibu wa barua yao kwenda kwa Balozi wa Marekani nchini, taasisi hizo zimedai, bendi hiyo ya muziki wa kizazi kipya, inapiga muziki wa Kiislamu.


“Kitendo cha bendi hiyo inayojinadi kuwa ni ya muziki wa Kiislamu, ni uchokozi na Waislamu wa Tanzania kamwe hawawezi kukivumilia.


“Muziki wa bendi hiyo ya Kiislamu kutumbuiza hapa nchini, ni jambo la hatari kwa Uislamu, hivyo tunapenda kukutahadharisha kuwa, ikiwa bendi hiyo haitazuiwa, likatokea la kutokea, ofisi ya ubalozi ndiyo itabeba lawama,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.


Hatua ya Waislamu hao kutaka kusitishwa kwa ujio na maonyesho ya bendi hiyo, kumetokana na matangazo mbalimbali kuwa itafanya onyesho la bure kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni.


Katika majibu ya Ofisa Mahusiano ya Jamii wa Ubalozi wa Marekani, Jeffery Salaiz, bendi hiyo ilikaribishwa nchini kwa ajili ya maonyesho mbalimbali visiwani Zanzibar wakati wa tamasha la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa wiki.


Ofisa huyo alisema, bendi ya Native Deen, inapiga muziki wa mahadhi ya hip hop na rap ikiutumia kufikisha ujumbe kwa vijana na kuwaasa wajali afya zao. 


Alisema, maonyesho hayo yamefanyika Mji Mkongwe wakati wa tamasha la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa wiki na kuhamasisha vijana dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kupitia Shirika la Kimataifa la Afya ya Familia chini ya mradi wa ujana. 


Ujio wa bendi hiyo ulidhaminiwa na Wamarekani na Mfuko wa Rais wa Marekani wa kusaidia kupambana na ukimwi.


Ofisa huyo alisema, maonyesho ya bendi ya Native Deen yanafanyika bure.


Hata hivyo, aliwahamasisha watu kusikiliza muziki wa bendi hiyo ya vijana wa Kimarekani wanaoamini katika Uislamu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents