Habari

Benki ya NMB imekabidhi zawadi kwa washindi tisa wa Kampeni ya MastaBoda (+Picha)

BENKI ya NMB imekabidhi zawadi kwa washindi tisa wa MastaBoda kama washindi wa wiki baada ya kufikisha miamala hamsini kupitia mfumo wa malipo wa MastercardQR katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Zoezi hilo liliendeshwa na Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi- Yusuph Achayo na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda- Michael Massawe.

Meneja Mahusiano wa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB – Yusuph Achayo (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu 50,000 dereva Bodaboda wa Kituo cha Kibamba Hospitali-Jonas Ruben. Akishuhudia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe.

MastaBoda ni kampeni inayoendeshwa na NMB kwa ajili ya kuwawezesha waendesha Bodaboda kuunganishwa katika mfumo wa kibenki ili waweze kupokea malipo kupitiamfumo wa Mastercard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na mfumo wa malipo wa Mastercard QR.

Akikabidhi zawadi hizo Achayo ametoa wito kwa waendesha Bodaboda ambao hawajajiunga na mfumo wa MastaBoda kujiunga ili kuendesha biashara zao kisasa kwa usalama wa fedha zao.

Nao washindi walioibuka na kitita cha Sh, 50,000. Wameimwagia sifa NMB kwa kutimiza ahadi, kwani zinawaongezea nguvu ya kupambana ili kufika mbali zaidi katika kuendesha biashara zao.

“Tangia nijiunge na mfumo huu, hii ni mara yangu ya pili kushinda, najisikia furaha sana. Tangu nianze kufanya miamala na QR nina amani, badala ya kutembea na pesa sasa fedha yangu inaingia moja kwa moja benki, mfumo huu pia unaookoa muda hasa katika kutafuta chenchi.”alisema Ebenezer Elisha (Mwenge) ambaye pia ni mmoja wa washindi.

Washindi wengine waliojizolea kitita hicho ni Goodluck Ntaya (Kawe Ukwamani),  Mohamed Abdallah (Buguruni Rozana)Twaliha Mfinanga(Rozani Mafleti) na Frorian Byabato (Roziani Mafleti).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents