Burudani

Benzema afunguka chanzo cha kutemana na Rihanna

Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema amefunguka na kuweka wazi sababu za yeye kutemana na mrembo Rihanna ni Chris Brown.

Rihanna na Karim Benzema

Benzema ambaye mwanzoni mwa mwaka 2015 alikuwa karibu sana na Rihanna na hata kuonekana naye kwenye fukwe na sehemu za starehe wakila bata, amesema ukaribu wao ulikuja kuvunjika baada ya mrembo huyo kuweka wazi kwamba ana hisia na ex wake yaani Chris Brown, hivyo asigependa kuja kumuumiza mbeleni hivyo ni heri watemane.

Tulikuwa marafiki kiasi chake lakini hakukuwa na mahusiano ya mapenzi,watu waliona urafiki wetu ni wa mapenzi lakini kwa bahati mbaya mambo hayakwenda hivyo. Rihanna aliniambia anampenda sana Chris hivyo angeishia kuniumiza tuu” Alisema Benzema kwenye mahojiano yake na Radio Marca ya nchini Hispania.

Hata hivyo Benzema alisisitiza kuwa kwa sasa wanawasiliana na Rihanna kama Kaka na Dada kwani tayari ana mchumba wake mpya aitwaye ‘Cora Gauthier ‘ na anampenda sana.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents