Burudani

Kylie Jenner ajirekodi akipata huduma ya dharura

Mwanadada Kylie Jenner aishangaza dunia kwa kujirekodi makatika tukio likimuonyesha akipatiwa huduma ya haraka ya hewa ya oxygen na kuweka katika mitandao ya kijamii.

Kylie Jenner alilazimika kupatiwa huduma ya kwanza ya hewa ya oxygen kutokana na tatizo la ngozi yake, akiwa yupo safarini nchini Amerika Kusini. Baada ya kupata nafuu Kylie alitumia matndao wa snapchat kujulisha mashabiki zake kuwa yupo sawa kwa sasa.

Picha na video zilimuonyesha Kylie akiwa amevaa kifaa ambacho kitamsaidia kupokea hewa hiyo ya oxygen aliokuwa akipatiwa na wahudumu wa afya ndani ya chumba cha hotel alichokuwepo.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Kylie, wamesema kwa sasa yupo nchini Peru, ambako alikuwepo tangu siku ya Jumanne ingawa sasa wapo hospital ta Lima.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents