Michezo

SportPesa wamkabidhi Waziri Mwakyembe Milioni 50 za Serengeti Boys (Video+Picha)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh Dk Harrison Mwakyembe leo amekabidhiwa hundi ya kitita cha Shilingi milioni 50 na Kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo ya SportPesa ili kusiaidia timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys.

Waziri Mwakyembe akikabidhiwa hundi ya Milioni 50 na Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Bw Abbas Tarimba

Waziri Mwakyembe wakati wa makabidhiano hayo amesema ameishukuru sana kampuni hiyo na kuahidi kuwa Serikali kupitia wizara yake itashirikiana na kampuni ya SportPesa ili kuweza kukuza michezo hapa nchini.

Kutokana na kutokuwa na mfumo mahususi wa kupata pesa ndiyo maana tunachangisha niwashukuru sana Abbas Tarimba ambae ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania na napenda niwahakikishie kuwa Wizara  itashirikiana na nyie“Amesema Waziri Mwakyembe.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Bw Abbas Tarimbo amesema wametoa fedha hizo ili kuonyesha watanzania kuwa ni kwa kiasi gani kuwa kampuni yao imejikita zaidi kunyanyua Soka la Tanzania.

Abbas Tarimbo akiteta jambo na Mwakyembe

SportPesa wametimiza ahadi yao waliyoitoa siku ya Uzinduzi ya  kutoa kitita cha Sh milioni 50 kusaidia juhudi za Serengeti Boys ili kufanya vizuri katika mechi za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON U-17 nchini Gabon.
Kampuni ya Sportspesa imetoka nchini Kenya ambako inadhamini vilabu vikubwa vya AFC Leopards ,Gor Mahia na Nakuru All Stars vinavyoshiriki ligi kuu ya Kenya.

SportPesa tayari wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kumalizana na Vilabu vya Yanga na Simba SC ili kukamilisha mikataba ya kudhamini Klabu hizo kongwe nchini Tanzania.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents