Burudani

BET kuwapa tuzo ya heshima Yvonne Chaka Chaka na Ilwad Elman

By  | 

Waandaaji wa tuzo za BET wamewatangaza watu wawili ambao watapokea tuzo ya heshima ya Global Good Power kwa mwaka huu.

Waliofanikiwa kutajwa ni mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka na Ilwad Elman raia wa Canada mwenye asili ya Somalia.

Kupitia mtandao wa Instagram wa waandaaji wa tuzo hizo wameandika, “This year we have two @BET_Intl#GlobalGood honourees! The first is social activist Ilwad Elman! @i_elman ??????.” “Our second @bet_intl #GlobalGood award goes to humanitarian Yvonne Chaka Chaka! ??????,” wameandika katika picha nyingine waliyoiweka katika mtandao huo.


Picha ya Ilwad Elman (Kushoto) akiwa na Kofi Anan katika mkutano wa vijana wa dunia wa One Young World

Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka jana kwa watu wanaotoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika na mtu wa kwanza kupatiwa tuzo hiyo alikuwa ni Miss Tanzania 2001, Millen Magesse na mwaka jana akipatiwa Akon kutokana na mradi wake wa kusambaza umeme wa jua ‘Akon Lighting Africa’ ambao umepanga kuleta maendeleo kwenye bara la Afrika.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments