Burudani

BET wampatia heshima kubwa Chance The Rapper

Jitihada huzaa matunda. Hatimaye waandaaji wa tuzo za BET wamefanikiwa kuona juhudi za Chance The Rapper na kuamua kumpatia heshima yake.

Rapper huyo ametangazwa kupatiwa tuzo ya Humanitarian Award ya BET siku ya utoaji wa tuzo hizo Juni 25 ya mwaka huu katika ukumbi wa Microsoft Theater mjini Los Angeles.

Chance amekuwa akijitolea katika mambo kadhaa ya kijamii ikiwemo kusaidia kukusanya zaidi ya dola milioni moja kwa ajili ya kuzisaidia shule za jumuiya za mjini Chacago.

Kwa mwaka jana muigizaji na mwanamitindo, Jesse William ndiye aliyefanikiwa kuipata tuzo hiyo. Kipengele cha tuzo hiyo kilianzishwa mwaka 2002 ambapo Muhammad Ali ndio alikuwa mtu wa kwanza kukabidhiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents