Habari

Bibi wa miaka 72 ajifungua nchini India

Mwanamke mwenye umri wa miaka 72 amejifungua mtoto wa kiume katika hospitali moja nchini India.

160511045718_daljinder_kaur_640x360_bbc

Mwanamke huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari na kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba, yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine blakini njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.

Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana, nchini India na matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.

Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79, tukio hilo limezua mjadala mkali kuhusu kutumiwa kwa teknolojia hiyo ya IVF na umri ambao wanawake wanaweza kuruhusiwa kuitumia kupata watoto.

Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo ni karibu miaka 55.

Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae.

“Ukimzaa mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua mtoto kisha uwaache watu wengine wakimlea,” alisema Dkt Nayar.

Ni mara ya pili kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70 alijaliwa mtoto nchini humo.

Lakini mwanamke huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents