Burudani

Bifu Mpya

O-Ten naye ameibuka na kuwatupia lawama baadhi ya Ma-Dj, akidai kwamba wamekuwa wakiacha kupiga nyimbo za wakongwe hao kwa kuwa hawatoi fedha.

Msanii huyo amesema jambo hilo limefanya Ma-Dj na wasanii wageuke maadui, hawapendani kama zamani.

“Unajua zamani ulikuwa unampa Dj wimbo wako anaupiga redioni bila kuombana rushwa, zaidi mnakuwa marafiki kama ndugu kwa kuwa mnategemeana, lakini sasa ukiuliza wasanii kumi, saba watakuambia wamejenga bifu na Ma-Dj,” anasema O-Ten.

Msanii huyo, ambaye amewahi kutamba na singo ya ‘Nicheki’ na wimbo wa ‘Sifa 10 za Demu’ anasema wasanii wakongwe husimamia wenyewe kazi zao na wanaona jambo hilo ni kero. “Hali ya sasa ni mbaya, kwa nini tusiishi kama zamani?” anahoji.

“Kuna siku nilidhani ni utani, nilipeleka kazi yangu kwa Dj fulani sipendi kumtaja jina, eti akaniomba fedha ya ‘promo’ ilinishangaza.

“Kama wanataka fedha ni bora wabainishe bei ili tufahamu kuwa mambo yamebadilika. Iwekwe wazi kwamba kupiga wimbo redioni ni kiasi kadhaa na kuwepo na risiti.”

Msanii huyo ambaye sasa anaandaa albamu mpya yenye jumla ya nyimbo 10, anasema hakujumuishwa katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Muziki za Kili kwa kuwa hakuwa na fedha za kutosha kutangaza singo yake. Msanii huyo aliyeanzia Kundi la East Coast, lililokuwa likiongozwa na King Craz GK na kuhamia Kundi la Family linaloongozwa na Chid Benzi kisha baadaye kufanya kazi binafsi amesema alikuwa akihama kutokana na bifu lakini sasa ameona mambo hayo hayafai.

“Bifu zinarudisha nyuma maendeleo ya muziki, mtu unapoteza mashabiki pia watu wanakudharau, sitaki tena mambo ya bifu,’ anasema O-Ten ambaye anatarajia kutua nchini Burundi na Rwanda kufanya maonyesho Juni mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents