Burudani

Blac Chyna aamua kurudi kwenye kazi yake ya zamani

By  | 

Blac Chyna ameamua kutafuta mkwanja zaidi na kuweka pembeni ugomvi uliopo kati yake na ex wake, Rob Kardashian.

Kwa mujibu wa TMZ, umeripoti kuwa mrembo huyo ameamua kurudi kwenye kazi zake za mwanzoni alizokuwa akizifanya kwa kutangaza katika klabu za usiku nchini Marekani.

Chyna anatarajiwa kuanza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye kazi yake hiyo ya katika klabu ya Medusa Lounge, mjini Atlanta Jumamosi hii.

Wakati huo huo siku ya Jumatatu ya Julai 17, video vixen huyo atakuwepo katika klabu ya Ace of Diamonds iliyopo West Hollywood ambapo anadaiwa kupokea kiasi cha dola 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 22 kwa fedha za kitanzania.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments