Burudani

Black Panther haikamatiki, yazidi kutikisa dunia kwenye mauzo

By  | 

Filamu ya ‘Black Panther’ inazidi kufanya vizuri katika mauzo yake duniani.

Kwa mujibu wa Box Office, mpaka sasa filamu hiyo imeingiza kiasi cha dola milioni 654,226,086 kwa Marekani.

Kutokana na kiasi hicho kilichoingiza filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Marvel Studios, imevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye box office.

Black Panther ambayo imeongozwa na Ryan Coogler, ilitumia bajeti ya kiasi cha dola milioni 200–210 katika kuitengeneza.

Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments