Michezo

Blatter: Kura ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 haikupangwa

Sepp Blatter ambaye alikuwa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA amesisitiza kuwa kura ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 haikupangwa ,amesema ”huwezi kununua kombe la dunia”.

Sepp Blatter Fifa

Blatter amesema hana hatia kufuatia madai ya ufisadi huku akingoja uamuzi wa rufaa yake aliyoikata dhidi ya marufuku ya miaka nane aliyopigwa na FIFA.

“Nina hakika kutakuwa na uamuzi wa haki na kwamba sijafanya uhalifu wa aina yoyote”. Alisema Blatter.
FIFA itafanya uchaguzi wa kumpata rais wake mpya mnamo tarehe 26 mwezi Februari.

Blatter ambaye alishinda kiti hicho kwa mara ya tano mfulilizo mnamo mwezi Mei lakini akapigwa marufuku kwa miaka minane kwa kumlipa pauni milioni 1.3 rais wa UEFA aliyesimamishwa kazi Michel Platini,malipo yanayodaiwa kuwa na utata.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents