Habari

Bomoa Bomoa Tabata Dampo

Wakazi wa maeneo ya Tabata Dampo wamekumbwa na sakata la bomoa bomoa ambayo imepelekea kuwaathiri kwa namna moja au nyingine, kutokana na kile kilichosemekana kuwa wakazi hao wamevamia maeneo ambayo ni ya mfanya biashara maarufu wa kampuni ya usafiri zamani Fresh ya Shamba.

Tabata Dampo

 

 

 

Wakazi wa maeneo ya Tabata Dampo wamekumbwa na sakata la bomoa bomoa ambayo imepelekea kuwaathiri kwa namna moja au nyingine, kutokana na kile kilichosemekana kuwa wakazi hao wamevamia maeneo ambayo ni ya mfanya biashara maarufu wa kampuni ya usafiri zamani Fresh ya Shamba.

 

 

 

Kizazaa hicho kilitokea siku chache zilizopita, ni baada ya wakazi wa eneo hilo kuwa na kesi na mfanya biashara huyo kwa zaidi miaka miwili ambapo suluhu haikuwa imepatikana, mpaka ilipofikia hatua ya kuwabomolea wakazi hao nyumba na kuwaacha katika mazingira magumu.

 

 

 

Akizungumza na bongo5.com mmoja wa wakazi wa eneo hilo bwana Ally Shundi ambaye alisema “tumekuja kubomolewa bila hata kupewa taarifa na hata siku ambayo watu wa bomoa bomoa walipokuja walijidai wanakuja kusafisha bara bara yao lakini cha kushangaza tunaona watu wanaanza kubomoa nyumba zetu, si bora wangetutaarifu mapema walau tukajiandaa lakini hawakufanya hivyo matokeo yake wanatutesa na pia wametuharibia mali zetu”

 

 

 

Aidha wakazi hao walichukua hatua ya kuandamana mpaka ikulu kwa ajili ya kuonana na Mheshimiwa Raisi lakini hawakuweza kuonana nae bali kilio chao kilisikilizwa na Mkuu wa mkoa Bwana Abbas Kandoro ambaye alitoa agizo la kuwataka warudi kwenye maeneo yao yaliyobomolewa mpaka tamko rasmi la serikali litakapopitishwa.

 

 

 

Tabata Dampo

 

 

 

Shirika la kutoa misaada la Msalaba Mwekundu (Red Cross) halikuwa nyuma katika kutoa misaada kwa wakazi hao kwa kuwapatia vitu kama mahema na chakula.

 

 

 

Bwana Kandoro aliwataka wakazi wa maeneo hayo kwenda kupatiwa viwanja, huko buyuni maeneo ya Chanika lakini waligoma wakidai kuwa hawako tayari kuondoka eneo hilo mpaka watakapolipwa fidia ya gharama za nyumba na mali zilizopotea na kuharibika, na mpaka sasa wakazi hao wametakiwa kuorodhesha gharama za nyumba zao na mali zilizoharibika tayari kwa kuanza taratibu za malipo.

 

 

 

Wakazi hao mpaka kufikia hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu sana mithili ya wakimbizi, pia upo uwezekano wa kuhatarisha maisha ya watoto wadogo kiafya na kisaikolojia kwani wengi wao kwa hivi sasa wanashindwa kuhudhuria masomo kama ilivyokuwa awali.

 

 

 

Tabata Dampo

 

 

 

Haikuishia hapo Mkuu wa Mkoa pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali wamewataka walioshiriki katika kubomoa kwenye makazi ya raia hao wafukuzwe kazi haraka iwezekanavyo.

 

 

 

[Video kutoka Tabata Dampo zitafuatia leo baada ya muda mfupi.]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents