Habari

Buff G ajichimbia kijijini, dah Iringa!

Buff G“lengo langu hasa la kukimbia mjini na kuja kujificha huku ni kwamba nahitaji utulivu wa hali ya juu kwani nimegundua mjini kuna mambo mengi kiasi kwamba utulivu kunakuwa hakuna ndio maana nimekuja huku kwa lengo la kutulia na…..”

Buff G


“lengo langu hasa la kukimbia mjini na kuja kujificha huku ni kwamba nahitaji utulivu wa hali ya juu kwani nimegundua mjini kuna mambo mengi kiasi kwamba utulivu kunakuwa hakuna ndio maana nimekuja huku kwa lengo la kutulia na kuandaa albam yangu binafsi kama Buff G mwenyewe” ni maneno yake Benjamin Gembe a.k.a Buff G.


Alikuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi la East Coast Team lakini yeye ndio alikuwa wa mwanzo kabisa kujiengua ndio wengine wakafuatia, pamoja na hayo kijana huyu ana vipaji kibao ikiwa ni pamoja na ubunifu wa mavazi, uchoraji, kutengeneza video, uandishi wa miongozo ya filamu (Script) n.k.


Akielezea maisha ya kijijini Buff alisema “Dah! Eh bana mi naenjoy big time kuwa huku kwani napata vitu vingi ambavyo mjini huwa sivipati, nakula vyakula fresh, matunda pia utulivu wa nafsi nataka nikitua mjini washabiki wa muziki wa Hip Hop waone kuwa mtu mzima kweli nilienda kupanga mashambulizi kikamilifu.


“unajua ni mambo mengi sana ambayo nimefanya katika gemu ya Hip Hop hata katika makundi ambayo nimewahi kuyaunda mimi na kushirikiana nayo lakini yote hayo nahitaji kusaau na kuwasamehe wale ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nafeli ila naahidi kuirudisha heshima na umuhimu wangu kwenye gemu”-Buff G.


Buff G amepania kufanya mapinduzi makubwa sana kwani amedai kuwa mwaka 2007 kwake ni wa maandalizi kisha 2008 ni mwaka wa harakati na vitendo na sio blah blah “kila mtu akija anadai atafanya mapinduzi then mapinduzi yenyewe hayaonekani that’s Bull Shit” alifoka Buff alipokuwa akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu.


Mwana hiphop huyu yuko mkoani Iringa katika moja ya vijiji vya ndani kabisa ambaco hakutaka kijulikane kwa kuhofia usumbufu na haijulikani ni lini mwisho wa likizo yake hiyo.


Amewahi kutamba na hibao kadha wa kadha kama vile ‘nitarudi, kumbe hata wewe’, na video kadhaa ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika medani ya mzini hapa nchini, tunakusikilizia mtu mzima.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents