Burudani

Bushoke aeleza mpango wa kusaini QS Mhonda ili kuungana na Q Chief ndani ya QS International Band

Msanii mkongwe wa muziki, Boshoke amesema ingawa kwa sasa anafanya kazi na Q Chief ndani ya bendi ya ‘QS Internalional Band’ lakini bado haja saini mkataba na bosi wa bendi hiyo.
Q Chief na Bushoke

Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Bushoke amesema kwa sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho kuhusu kusaini.

“Kusema kweli bado tupo kwenye mazungumzo ya mwisho juu ya uwepo wangu ndani ya QS International Band, lakini kila kitu kipo sawa” alisema Bushoke.

Aliongeza, “Nadhani kila kitu kikiwa sawa nitaweka wazi kila kitu juu ya mkataba, lakini kwa sasa bado ndio maana nashindwa kuzungumzia. Lakini tayari nimeshaanza kufanya kazi, kuna kama show tano hivi tumefanya pamoja na Q Chief,”

Katika hatua nyingine Bushoke wamewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria kazi zake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents