BurudaniVideos

Ilikuwa ngumu kuwashawishi wazazi kuwa rapper – Chemical

Haikuwa rahisi kwa rapper Claudia Lubago, aka Chemical kuwashawishi wazazi wake kuendelea na career ya muziki wa hip hop wakati akisoma.

Akiongea na Bongo5, rapper huyo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Fine Arts and Performing, amesema wazazi wake hawakumwelewa mwanzo.

“Sasa hivi wanasupport lakini mwanzo ilikuwa ngumu,” anasema.

“Wazazi wote walikuwa wagumu kukubali kwasababu nyumbani kwetu watu wengi wanasoma kwahiyo mimi nilionekana kidogo kama naenda sehemu tofauti. Lakini ilibidi nielewe sababu kila mzazi anataka kitu bora kwa mwanae. Kwahiyo niliamini kuwa walikuwa wanataka nisome. Nilijitahidi nifanye vizuri kwenye masomo ili at least wakiniona nafanya muziki wasione kwamba muziki ndio unanifanya nifeli,” ameongeza.

“At the end of the day wakaona anafanya vizuri darasani, anajitahidi kwenye masomo, basi afanye.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents