Michezo

CAF yampa ulaji Muhsin Rajab kuisimamia Uganda dhidi Sudan ya Kusini CHAN

Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” limemteuwa Mkufunzi wa waamuzi kutoka Zanzibar Muhsin Ali Rajab ‘Kamara’ kusimamia mchezo wa kufuzu CHAN kati ya Uganda Cranes dhidi ya wageni wao Sudan ya Kusini.

Mkufunzi wa waamuzi kutoka Zanzibar Muhsin Ali Rajab ‘Kamara’

Hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa Shirikisho hilo CAF.

CAF imempanga Kamara kusimamia mchezo huo utakaofanyika kwenye dimba la Namboole nchini Uganda akiwa sambamba na waamuzi kutoka Tanzania bara.

“Nashkuru Mungu kupata fursa hii ya kuwasimamia Waamuzi wa Tanzania bara, zamani ilikuwa Zanzibar na Tanzania bara katika soka sote wamoja sasa na tunasimama kama Tanzania”. Alisema Kamara.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents