Habari

Canada: Daktari atumia mbegu zake za kiume kama tiba 

Shirika moja la udhibiti wa matibabu nchini Canada limempokonya rasmi leseni daktari mmoja wa rutba ya uzazi aliyestaafu ambaye alitumia mbegu zake za kiume kuwapatia ujauzito wanawake wasioweza kushika mimba.Dr Norman BarwinMalalmishi yaliowasilishwa yanadai kwamba Dkt. Norman Barwin aloitumia mbegu zake za kiume kuwashikisha ujauzito wagonjwa wake

Chuo kikuu cha madaktari wa maungo na upasuaji cha Ontario kilitaja vitendo vya daktari Norman Barwin kuwa vya ‘aibu kubwa’.

Shirika hilo lilianzisha uchunguzi kuhusu madai dhidi yake mwaka 2016. Madai hayo yalianzia mwaka 1970 na yanashirikisha wagonjwa kutoka kliniki mbili za rutba ya uzazi mjini Ontario.

Akizungumza kwa niaba ya bodi ya jopo la nidhamu katika shirika hilo mjini Toronto siku ya Jumanne, bwana Steven Boldley alisema kuwa ya shirika hilo kwa bahati mbaya halikuweza kumchukulia hatua kali daktari huyo isipokuwa kumpokonya leseni yake mbali na kumtoza faini.

”Ulisaliti uaminifu wa wagonjwa wako na kupitia vitendo vyako uliathiri watu binafsi na familia zao na kusababisha uharibifu mkubwa ambao utaendelea kuwepo kwa vizazi vijavyo”, alisema.

Akiwa na umri wa miaka 80, daktari Barwin hakuwepo mbele ya jopo hilo la nidhamu na aliwakilishwa na wakili wake.

Hajawahi kutibu mgonjwa tangu 2014>

Taasisi hiyo iliandika visa 13 ambapo Dr Barwin alitumia mbegu zake za kiume kuwashikisha ujauzito wagonjwa wake. Wakili wa daktari huyo hakupinga madai hayo kwa niaba ya mteja wake.

Je Dkt Barwin anakabiliwa na madai gani?

Kulingana na taarifa ya vitendo alivyotekeleza iliotolewa na chuo hicho, kulikuwa na visa 13 ambapo Dkt. Barwin alitumia mbegu zake za kiume kuwapatia ujauzito wagonjwa wake.

Carolyn Silver, ambaye ni kaimu mwendesha mashtaka wa chuo hicho alikitaja kitendo cha Dkt. Barwin kuwa ‘kisichoweza kusameheka’.

”Vitendo vyake vya kushangaza vitawacha doa katika kazi hii”, aliambia jopo hilo siku ya Jumanne .

Dkt. Barwin awali alipigwa marufuku kwa muda na kutozwa faini na taasisi hiyo 2013 kwa kuwadunga wagonjwa watatu mbegu za kiume zisizo sawa.

Shirika hilo la udhibiti wa matibabu hatahivyo lilifanya uchunguzi wa hivi karibuni baada ya malalamishi kuwasilishwa kupitia madai kwamba watoto kati ya 50 hadi 100 walizaliwa kutokana na mbegu za Dkt. Barwin na kwamba 11 kati ya watoto hao walikuwa na jeni zinazofanana na daktari huyo wa maswala ya rutba ya uzazi.

Madai yote yaliowasilishwa dhidi yake hayajajaribiwa katika mahakama ya kiraia.

Je waathiriwa walisema nini?

Jopo hilo liliambiwa kwamba kulikuwa na taarifa zenye ushahidi mkali kutoka kwa waathiriwa wanne wa Dkt. Barwin.

Rebecca Dixon , ambaye familia yake inamshtaki Daktari huyo alisema kuwa , utambulisho wake ulihojiwa wakati alipofika umri wa miaka 25 ambapo aligundua kwamba Dkt. Barwin ndiye aliyekuwa babake.

Davina na Daniel Dixon” Familia ya Dkt Dixon iligundua kuwa Daniel hakuwa babake Rebeca

Familia hiyo ya Dixons iliwasiliana na Dkt. Barwin mwaka 1989 kuwasaidia kupata ujauzito na Rebecca alizaliwa mwaka mmoja baadaye.

Bi Dixon anasema kuwa wazo kwamba Dkt Barwin ndiye babake lilimfanya kujihisi ”mchafu”.

Anasema kuwa madhara ya vitendo vyake yamo ndani ya jeni zake na kwamba ni kitu ambacho siku moja atakipitisha kwa watoto wake.

Bi Dixon anasema kuwa ana ndugu 15 wa kambo tangu alipogundua kuhusu asili yake ya kibaiolojia.

Mgonjwa mwengine Dkt. Baldwin ambaye utambulisho wake unalindwa na sheria ya kupiga marufuku chapisho lake aligundua kwamba mbegu za kiume za mtu asiyejulikana zilitumika kumpatia ujauzito wakati alipotafuta usaidizi kutoka kwa Dkt. Barwin.

”Nilihisi kufanyiwa uhalifu – mchafu kama ambaye nilikuwa nimebakwa”, alisema baada ya kugundua alidungwa jeni za mtu asiyemjua.

Kwa mujibu wa shirika la habari BBC,  Baba mmoja ambaye utambulisho wake pia umefichwa , alielezea uchungu aliokuwa nao wakati alipogundua kwamba watoto wake hana uhusiano nao.

”Fikiria kuwaona wayoto uliodhani kuwa wako wanakuwa wakifanana na mtu mwengine”, alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents