Burudani

Cardi B aweka wazi siku ya kuachia albamu yake mpya ‘Invasion of Privacy’

By  | 

Cardi B ameweka wazi siku rasmi ya kuachia albamu yake ya kwanza ambayo ameipa jina la ‘Invasion of Privacy’.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa anaonekana kukikaribia kiti cha umalkia wa muziki wa Hip Hop, amethibitisha kupitia mtandao wa Twitter kuwa albamu hiyo itatoka April 6 ya mwaka huu.

“My album “INVASION OF PRIVACY” will be out APRIL 6!👌🏽👌🏽Thanks for the love❤️,” ameandika.

Miongoni mwa ngoma ambazo zinatarajiwa kusikika katika albamu yake hiyo ya kwanza ni pamoja na Bodak Yellow (Money Moves) na ‘Bartier Cardi’.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments