Michezo

CEO wa zamani wa Microsoft, Steve Ballmer ndio mmiliki mpya wa timu ya LA Clippers

Timu ya kikapu ya Los Angeles Clippers imepata mmiliki mpya.

nba_g_steveb2_cr_600x400
Steve Ballmer (kushoto akiwa na kamishna wa NBA, Adam Silver mwezi May) ndiye mmiliki mpya rasmi wa Clippers

Mwenyekiti Mtendaji wa zamani wa kampuni ya Microsoft, Steve Ballmer ameshinda dau la kuinunua timu hiyo kutoka kwa Shelly Sterling, mke wa mmiliki wa zamani wa timu hiyo, Donald Sterling.

Ballmer, ameinunua timu hiyo kwa dola bilioni 2. Ameichukua timu hiyo baada ya wiki kadhaa za mvutano wa kisheria kati ya Shelly and Donald Sterling, bilionea mwenye miaka 80 ambaye mapema mwaka huu alipigwa marufuku kujihusisha na NBA kwa kuongea kauli za kibaguzi dhidi ya watu weusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents