Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Chodry ataja sababu iliyochelewesha kutoka kwa filamu ya ‘Return to Zero’

Msanii kutoka kiwanda cha Bongo Movie, Diana Nsumba maarufu kama Chodry ameeleza sababu iliyofanya filamu yake mpya ya ‘Return to Zero’ ichelewe kutoka.

Professo-Jay

Chodry ni miongoni mwa wasanii chipukizi kwenye filamu waliotengeneza jina kwa muda mfupi kutokana na kufanya vizuri kwenye filamu nyingi na mastaa wakubwa ikiwemo, ‘Julieth’, ‘Only You’, ‘The Same Script’ na nyingine nyingi.

Akiongea na Bongo5, Chodry amesema, “Nilipanga kuachia filamu yangu mpya ya ‘Return to Zero’ tangu mwezi Aprili mwaka huu.”

“Kuna matatizo kidogo yakajitokeza ndio maana ikashindikana kutoka kwa muda muafaka, ila kwa sasa nashukuru kila kitu kipo sawa na filamu imetoka leo ipo mitaani. Filamu imetoka chini ya kampuni ya Steps Entertainment,” ameongeza.

Filamu ya ‘Return to Zero’ imefanikiwa kuchezwa na mastaa kadhaa wa kiwanda cha filamu Bongo akiwemo Hemedy PHD na wengine wengi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW