DStv Inogilee!

Chungwa langu lishaiva wazee…!!

Msanii Suma Ismail Sadiq (SUMA LEE) mwenye maskani yake mkoani Tanga, amekamilisha albam yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina la CHUNGWA..


Msanii Suma Ismail Sadiq (SUMA LEE) mwenye maskani yake mkoani Tanga, amekamilisha albam yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina la CHUNGWA,ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Bongo Flava albam hiyo pia itapatikana yote kwenye ringtones zitakazokuwa zikiuzwa na kampuni ya StarFish Mobile.

Suma Lee

Akiongea alipotia timu ndani ya ofisi zetu,Manager wa msanii huyo Paul Beda alisema taratibu zote zimekwishakamilika na albam hiyo (CHUNGWA) itakuwa mtaani katikati ya mwezi April.

Akiendelea alisema albam hiyo itakayokuwa na track 9 itakuwa noma yenye ladha tamu kama chungwa huku ikiwa imebeba ujumbe na mashairi ya kufa mtu na kusisitiza kuwa atakayeikosa basi atakuwa amefanya kosa kubwa ktk maisha yake kwa mwaka huu.

Alizitaja track hzilizopo ndani ya albam hiyo kuwa ni;Chungwa,Mnajistukia,Baa na Maa ft. Enika,La La Laa,Nisikiize ft. G-Square,Rafiki,Chungwa (rmx),Tofauti Sana na Chagua Lake.

Kazi nzima ya utengenezaji wa albam hiii umefanyika ndani ya studio za G2 chini ya producer Roy na kusimamiwa na Paul Beda.

Kabla ya kuamua kutoka kivyake Suma Lee alikuwa kwenye kundi la Park Lane pamoja na mwenzake Ilunga Khalifa a.k.a Cp a.k.a Cpwaa a.k.a Cha Pombe…ambapo walitamba sana na masongi kama vile Aisha pamoja na Nafasi Nyingine.

Albam itasambazwa na JFM wakisimamiwa na U&I Entertainment pamoja na G2 Records.

Wakati huo huo Manager huyo alisema wanatarajia kurelease video 2 mpya za msanii huyo hivi karibuni na kuzitaja video hizo kuwa ni za track Chaguo lake na Lalala huku kazi nzima utengenezaji wa video hizo ikiwa ni ya Chapakazi Filmz chini ya Adili a.k.a Hisabati.

 

  • SOURCE: Darhotwire

{mos_sb_discuss:10}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW