Michezo

Arsenal yapata pigo jingine jipya

Klabu ya Arsenal itamkosa kiungo wake wa kati Santi Cazorla hadi Machi mwakani, meneja wake, Arsene Wenger ameleeza.

hi-res-72691e3dd61baaaaecea47125f14ebee_crop_north

Mchezaji huyo anayechezea timu ya taifa ya Hispania, aliumia goti wakati wa mchezo kati ya Arsenal na Norwich ulioisha kwa sare ya 1-1. Klabu hiyo tayari ina majeruhi kiungo wao mwingine wa kati Francis Coquelin atakayekaa nje miezi mitatu baada ya kuumia goti.

Beki wa kati Laurent Koscielny na mshambuliaji Theo Walcott wameshapona majeraha yao na watarejea uwanjani.

Alexis Sanchez anauguza jeraha la misuli ya paja baada ya kuumia dhidi ya Norwich, huku Wenger akilazimika kutetea uamuzi wake wa kumchezesha mechi hiyo.

“Mimi si mtaalamu, lakini mkitaka kunilaumu, ni sawa.” alisema Arsene Wenger.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents