Burudani

Collo afunguka kuhusu matumizi ya kilevi

By  | 

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Collo ambaye alikuwa akifanya muziki wa rap, amefunguka juu ya jitihada alizopambana nazo katika kuhakikisha anaacha kutumia kilevi.

Collo ambaye kwa sasa anafanya muziki wa injili na tayari mwaka jana ameachia wimbo wake wa kwanza, amelieleza Jarida la Parents la nchini humo juu ya jitihada alizopambana nazo katika kuhakikisha anaacha kutumia kilevi hadi kumpokea Mungu katika maisha yake.

Msanii huyo pamoja na mkewe wameeleza mambo mbalimbali  kupitia  Jarida hilo kuhusu  maisha yao ya zamani na sasa.

Huyo sio msanii wa kwanza nchini humo kuamua kumrudia mungu, pia kuna msanii kama Lady Bee ambaye aliachana na muziki wa dunia na kuamua kufanya injili.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments