Michezo

Done Deal: Mshambuliaji hatari wa Ufaransa atua rasmi Arsenal

Klabu ya soka ya Arsenal ya nchini Uingereza imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette kutoka Olympique Lyonnais ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Arsenal ambapo usajili wake umevunja rekodi katika timu hiyo baada ya kununuliwa kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 53 na huenda ikafikia paundi milioni 60 kulingana na vipengele vilivyowekwa kutokana na kiwango chake atakachokionyesha uwanjani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Lacazette ameonyesha kufurahishwa kujiunga na Arsenal, kwa kuandika, ” Im so glad to join Arsenal Thank you for your trust and confidence Im excited to joining my new teammates and playing on this incredible Emirates Stadium ?⚪️.”

Awali Mesut Ozil ndio alikuwa akishikilia rekodi ya kusajiliwa kwa fedha nyingi na Arsenal mwaka 2013 akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 42.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents