Michezo

Conor McGregor ataushangaza ulimwengu – Page

Bingwa wa uzito wa kati nchini Uingereza, MichaelVenom” Page anaamini kuwa endapo, Conor McGregor akishinda pambano lake dhidi ya bingwa wa dunia, Floyd Mayweather basi anastahili kuwa mpiganaji wa wakati wote.

McGregor ambaye anakabiliwa na pambano kali na lakusisimua dhidi ya Mayweather Agosti 26 huko Las Vegas anahitaji kuitikisa dunia kwa kumpiga mpinzani wake huyo ambaye alishawahi kutangaza kustaafu mchezo huo.

Page, ambaye pia ni mtaalamu wa michezo ya martial artist anaamini dunia itashangazwa na matokeo yatakayo patika katika mchezo huo.

Bondia wa Uingereza, Michael “Venom” Page

“Nafikiri jambo la mwisho litakalo itikisa dunia baada ya lile la klabu ya Leicester kuchukua ubingwa Uingereza ni McGregor kumpiga mpanzani wake.

“Usiku mmoja tutashuhudia kivuli chake katika ulingo atakuwa mpiganaji wa muda”,alisema Michael “Venom” Page

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents