Copa Coca Cola Kuibua Vipaji

coca_m.jpgMashindano ya soka ya Copa Coca Cola yanatarajiwa kuanza keshokutwa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya kukamilika kwa hatua zote muhimu ambazo zilikuwa zikisubiriwa kwa hamu sana na mashabiki.

coca_1.jpg

Timu za mikoa za Tanzania Bara na Zanzibar zimepania kuchuana vikali katika mashindano hayo yanayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Michuano hiyo kwa kiasi kikubwa inatakiwa kusaidia kuweza kupata vijana wadogo wa kusakata soka ukizingatia ni kipindi kirefu kumekuwa hakuna mashindano yanayowahusisha vijana kitaifa.

Mashidano ya mwaka jana yalikuwa na dosari kadhaa ambazo ingekuwa vyema zingefanyiwa kazi katika mashindano ya mwaka huu na tatizo kubwa lilikuwa ni baadhi ya timu kuleta wachezaji wenye umri mkubwa katika michuano jambo ambalo safari hii litadhibitiwa kikamilifu.

Malengo ya mashindano hayo ni kutafuta vijana wazuri na wadogo ili waweze kuchezea timu ya taifa katika siku za usoni.

Hata hivyo, bahati timu iliyopatikana katika mashindano yaliyopita haijaweza kutumiwa vyema, baada ya kushiriki katika mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika nchini Burundi, mwaka jana.

Itakuwa vizuri iwapo Copa Coca Cola watatimiza malengo yake kwani inapendeza sana kuona timu zetu zikishiriki katika mashindano ya kimataifa.

Itapendeza sana kama TFF nao wakahakikisha wanajipanga vyema na kushirikisha timu zetu za vijana katika michuano mbali mbali ya kimataifa ili kuitangaza Nchi yetu.

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents