Michezo

Cristiano Ronaldo sasa anataka watoto saba

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametoboa siri kuwa anataka watoto wanne zaidi kufikisha idadi ya saba kulingana na namba ya jezi yake.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 mpaka sasa anawatoto watatu, Cristiano Jr mwenye umri wa miaka saba akifatiwa na pacha Eva na Mateo, na hivi karibuni amethibitisha kuwa mchumba wake Georgina Rodriguez ni mjamzito.

 

Nyota huyo ameweka wazi kuwa mtoto wake wa kwanza anahitaji wadogo zake sita ili kufikia jina la kibiashara la Cristiano ‘CR7’ ikiwa ni jezi yake anayovaa akiwa uwanjani.

Ronaldo alitoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha luninga cha Chinese TV iliyotumia gazeti moja la Ureno katika mahojiano hayo.

Gazeti hilo la kila siku la Ureno, Correio da Manha lilimnukuu Cristiano: “Cristianinho ni mwenye furaha.

“Anaendelea vizuri na amesema anataka wadogo zake zaidi. Ataka wawe saba, ni namba ya maajabu, nafiriki hilo ni zuri zaidi,” alisema baba wa mtoto huyo Ronaldo.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents