Burudani ya Michezo Live

Daily Mail kumlipa Melanie Trump $2.9m kufuatia kuandika habari ya kumchafua

Gazeti maarufu la Uingereza, The Daily Mail limemuomba radhi mke wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Melania Trump na kukubali kumlipa fidia kumaliza kesi iliyofunguliwa baada ya kuandika habari ya uongo kuhusu kazi yake kama mlimbwende.

Trump atalipwa dola milioni 2.9 kama fidia kutokana na madhara yaliyotokea.

“We accept that these allegations about Mrs. Trump are not true and we retract and withdraw them. We apologize to Mrs. Trump for any distress that our publication caused her,” Daily Mail na Mail Online wamesema kwenye maelezo yao.

Trump alifungua kesi dhidi ya Mail Online September mwaka jana akiwatuhumu kuandika habari ya kumchafua. Kwenye mashtaka yake alitaka alipwe dola milioni 150.

The Daily Mail ni gazeti la udaku nchini Uingereza lakini website yake inasomwa sana Marekani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW