Michezo

Daniel Sturridge (Liverpool) Nipo single lakini siwezi kusema ‘No’ kwa Rihanna

Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge amesema yupo single lakini kama mrembo Rihanna akimtaka kimapenzi, kamwe hawezi kumtolea nje.

Liverpool v Norwich City - Premier League

Akiongea na jarida la Life+Times linalomilikiwa na Jay Z, Sturridge aliongea masuala mengi kuanzia kuondoka Merseyside, maisha yake nje ya uwanja na mapenzi pia.

“Maisha yangu yamejikita kwenye football na hivyo ndivyo nahisi itakuwa mpaka nitakapostaafu. Lakini siku zote kuna muda wa mapenzi na kuvutiwa— nipo single, au sio? Sitasema hapana kwa Rihanna,” alisema mshambuliaji huyo.

d3bdf9c2382b11e3b0f722000a9f18db_8

Rihanna alikuwa na ziara nchini Uingereza mwezi uliopita ambapo Sturridge alihudhuria moja ya show zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents