Michezo
David Beckham amepewa tuzo ya Legend of Football
Mchezaji mkongwe wa soka duniani David Beckham ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa England amedhihirisha kuwa alitumia vyema nafasi yake akiwa uwanjani na kujenga jina na heshima kwenye soka ambayo itamfanya akumbukwe duniani.
Beckham ambaye alizichezea klabu za Manchester United na Real Madrid,Ac Millan,PSG ametunikiwa tuzo ya heshima kama ishara ya kuutambua mchango wake kwenye soka duniani.
Tuzo hizo za 20 ambazo hujulikana kama Legend of Football Award alipewa na wanachama wa kamati ya Football Extravaganza na alipewa katika ukumbi wa The Grosvenor House London usiku wa Septemba 1.
Tuzo hiyo pia wamewahi kupata watu mbali mbali kwenye list hiyo chini.