Habari

Dawa ya kupunguza makali ya HIV zaboreshwa

Watafiti kutoka nchini Uingereza wamebaini namba ya kuboresha dawa za kupunguza makali ya virusi vinavyosababisha ukimwi, katika bara la Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Watafiti hao wamesema kwamba, kiasi cha watu wenye Virusi vya UKIMWI wana uwezo wa kuishi sawa kama watu wengine wasio na virusi hivyo endapo watatumia dawa hizo na kuzingatia maelekezo.

Hata hivyo wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha Bristol, walifanya uchunguza kwa watu wenye virusi vinavyosababisha UKIMWI wapatao elfu tisini. Makadirio yalionyesha kuwa,mtu mwenye umri wa miaka 21 aliyeanza matibabu mwaka 2008 au aliyeanza baada ya mwaka huo anaweza kuishi mpaka kufikia umri wa miaka 70.

Kwa upande wa Takwimu zinaonyesha kuwa watu walioathirika na virusi hivyo ni milioni 36, wengi wao wakiwa barani Afrika, na kwa upande wa Ulaya na Amerika Kaskazini ni watu milioni mbili.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents