Michezo

VIDEO: Real Madrid watinga ‘kinyonge’ fainali ya Klabu bingwa Ulaya

Klabu ya Real Madrid jana usiku imefuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) kwa mara ya pili mfululizo licha ya kufungwa bao 2-1 na Mahasimu wao Atletico Madrid.

Mashabiki wa Atletico wakiwazomea Real Madrid juu kwenye picha baada ya kipigo

Mabao mawili ya haraka haraka ndani ya dakika 16 za mwanzo kutoka Saul Niguez na Antoine Griezmann yaliishtua Real kabla ya Isco kuwatuliza kwa bao lililowavunja matumaini wenyeji muda kuelekea ukingoni mwa kipindi cha kwanza.

https://youtu.be/zXo1CxqAO1Y

Real Madrid wameungana na Juventus kutinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 ukijumlisha na ya mechi ya kwanza ambayo Madrid walishinda goli 3-0.

Fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya itachezwa mwezi ujao June ya tarehe 3 kunako Dimba la Cardiff huko Uingereza.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents