Burudani

Dela aeleza sababu ya kushirikiana na Timmy Tdat kwenye ‘We’ll Be Ok’

By  | 

Msanii wa Kenya Dela amefunguka sababu ya kufanya kazi na Timmy Tdat kutoka lebo ya Kaka Empire inayomilikiwa na rapper King Kaka.

Wasanii hao wameachia wimbo wao mpya wa pamoja uitwao ‘We’ll Be Ok’. Akiongea na Bongo5, Dela ambaye pia amewahi kuimba cover ya wimbo wa Hello wa Adele, amesema kuwa ni siku nyingi alikuwa anatamani kufanya kazi na Timmy kabla hawajakutana studio.

“Nimekuwa shabiki wa Timmy tangu “Wele Wele”. Nilikuwa natamani kufanya naye kazi pamoja. Tulikutana Pacho studio na alitaka kufanya kazi nami pia. Tulijichochea kwa nyimbo chache, na tulipata kuzungumza. Tulitaka kuonyesha kwamba watu kutoka asili tofauti wanaweza kuwa sambamba na hushinda upendo hushinda matatizo yote ya fedha au vinginevyo,” amesema Dela.

Usikilize hapa chini wimbo huo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments