Dereva wa Wangwe Apandishwa mahakamani

Kijana Deus Mallya (27) anayedaiwa kuwa dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe wakati wa ajali, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakaimu Mkazi Dodoma, chini ya ulinzi mkali.

Kijana Deus Mallya (27) anayedaiwa kuwa dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe wakati wa ajali, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakaimu Mkazi Dodoma, chini ya ulinzi mkali.

Mallya ambaye ni mtuhumiwa namba moja wa ajali hiyo, anashitakiwa kwa makosa mawili ya kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo na kuendesha gari bila leseni. Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mallya anadiwa kutenda makosa hayo saa 2:30 usiku katika eneo la Panda Mbili, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma Julai 28, mwaka huu.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka hayo mnamo saa 1:00 asubuhi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Moses Mzua, Mallya alikana tuhuma zote. Katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka, Mallya anadaiwa kutenda makosa hayo mawili na kusababisha kifo cha Mbunge Waangwe.

Hati hiyo ya mashitaka iliyosomwa na Hakimu Mzua, inaonyesha kwamba Mallya alitenda makosa hayo mawili katika barabara ya kutoka Dodoma kwenda Morogoro.

Mallya ambae aliruhusiwa juzi kutoka Mospitali ya Mkoani wa Dodoma ambako alikuwa amelazwa tangu ilipotokea ajali hiyo, alirudishwa rumande katika Gereza la Isanga hadi kesi yake itakapotajwa tena Agosti 14, mwaka huu. Mkemia Mkuu Katika hatu nyingine, taarifa kutoka duru za polisi mkoani hapa zinaeleza kwamba, baadhi ya sehemu za mwili wa marehemu Wangwe zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dares Salaam kwa uchunguzi wa kimaabara ili kujua chanzo cha kifo cha mbunge huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Omary Mganga, alipoulizwa na gazeti hili mjini hapa jana, alisema uchunguzi bado unaendelea na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baada ya kazi hiyo kukamilika. Mganga alifafanua kwamba, uchunguzi huo ni mpana na kwamba unahusisha wataalamu na idara tofauti ikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu hivyo ni vema watu wasubiri mpaka utakapokamilika.

“Uchunguzi bado unaendelea, sisi tunapata taarifa tofauti kutoka kwa watu mbalimbali, sasa tunaweza kusema ni hivi kumbe ni vile, kwa hiyo subirini tufanye uchunguzi kisha tutaona ukweli uko wapi na tutatoa taarifa za kina,” alisisitiza kamanda Mganga.

Alisema kukiwa na taarifa nyingi tofauti, zitaweza kuwachanganya wananchi hivyo ni vema ikasubiriwa kufanyika uchunguzi makini na kitaalamu ili kuweza kupata ukweli kuliko kuanza kuhisi. Kifo cha Wangwe kimegubikwa na utata kutokana na mazingiria yeke ambayo yamesababisha wananchi wa jimbo lake la na wanafamilia, kukataa mwili huo usizikwe ili kutoa fursa ya kufanyika uchunguzi wa kina kitaalamu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents