Awards

Diamond, Davido wagaragazwa na msanii kutoka Uganda kwenye tuzo za Nickelodeon

Jana usiku nchini Marekani kulikuwa na ugawaji wa tuzo za kimataifa za Nickelodeon ambapo mastaa nguli kutoka Afrika walikuwa wanachuana kuwania tuzo hizo.

Eddy Kenzo

Mastaa hao ni Diamond Platnumz, Cassper Nyovest, Davido, Emannuella na Eddy Kenzo ambao wote walikuwa wanachuana kwenye kipengele cha Favourite African Star 2018 ambapo Eddy Kenzo ameibuka kidedea kwa kunyanyua tuzo hiyo.

Tuzo hiyo ambayo watu wengi walibashiri kuwa mtoto mwenye kipaji cha kipee barani Afrika, Emmanuella angeibuka kidedea, imezua gumzo nchini Nigeria kwa watu wengi kuhoji ushindi wa Eddy Kenzo.

Tazama orodha kamili ya washindi wote wa tuzo hizo HAPA

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents