Michezo

Mtoto wa George Weah, Timothy awavunja moyo Waliberia

Kwa mara ya kwanza mtoto wa Rais wa sasa wa Liberia na mchezaji nguli wa soka wa zamani, Timothy Weah ameichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya wakubwa ya Marekani.

                                                      Timothy Weah

Timothy (18) ambaye anacheza katika klabu ya PSG aliingia katika dakika ya 86 kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Bobby Wood ambaye alifunga bao lililoipa Marekani ushindi dhidi ya Paraguay kwenye mchezo huo wa kirafiki.

Kutokana na kuchezea timu ya taifa ya Marekani, Timothy hataweza tena kuichezea timu ya taifa ya Liberia na kuwafanya mashabiki wa taifa hilo kunyong’onyea kutokana na ndoto zao walizokuwa wameziweka kwa mchezaji huyo.

Timothy alizaliwa katika mji wa New York na aewahi kuichezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Marekani jumla ya mechi 14 na amefunga mabao sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents