Burudani

Diamond na Wizkid kuitikisa Afrika muda wowote na kolabo yao, wenyewe watoa neno (+Video)

Kama ulikuwa unasubiri kolabo ya wasanii maarufu zaidi barani Afrika, Wizkid na Diamond Platnumz basi ondoa hofu kwani wawili hao wamethibitisha kuwa wamefanya kolabo na wanatarajia kuachia wimbo huo very soon!.

Diamond na Wizkid

Wizkid ndiye aliyethibitisha taarifa hizo, kupitia video fupi aliyoiweka Diamond kwenye StoryLine yake ya mtandao wa Instagram, StarBoy amesema kuwa kuna kazi inakuja very soon na mashabiki wao wakae mkao wa kula.

Wizkid na Diamond Platnumz wamekutana mjini Dubai kwenye Tamasha la One Africa Music Fest, ambapo mastaa kibao walihudhuria kwenye tamasha hilo la kimataifa.

Hakuna ubishi kuwa kolabo hiyo, huenda ukawa wimbo mkubwa sana barani Afrika kwani kolabo nyingi za Diamond alizofanya na wasanii wakubwa wa Nigeria hazijawahi kumuangusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents