Dida Matatani

Dida Matatani
Inasemekana kwamba mtangazaji maarufu wa Times FM, Dida wa Mchops (Hadija Shaibu), alisimamishwa na kukamatwa na Polisi Jumatano huko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere akijiandaa kupanda ndege kuelekea China.

Inasemekana kuwa baada ya Dida kukamatwa, alipelekwa kwenye choo maalumu kilichopo uwanjani hapo ambacho hutumiwa na askari wa kitengo hicho kuwahifadhi watuhumiwa wanaowakamata wakiwa wamemeza dawa za kulevya kwa muda ambapo endapo mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo atazitoa wakati akijisaidia.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa tangu alipoingizwa kwenye choo hicho juzi jioni hadi jana saa nne asubuhi, hakuweza kugundulika kuwa na dawa hizo tumboni ambapo alichukuliwa hadi makao Makuu ya Kitengo hicho, huko Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuhojiwa.

Taarifa nyingine zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Dida alidhaminiwa jana majira ya saa kumi jioni.

Pole sana Dida na yaliyokukuta!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents