Habari

Dina Marious airejesha tena Kitchen Party Gala

Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo cha EFM, Dina Marious ameirejesha tena Kitchen Party Gala – hafla ambayo huwakutanisha wanawake mbalimbali nchini kuzungumza masuala ya mahusiano, familia, kujikwamua kiuchumi na mengine.

20151029010921

“Kila mwanamke ana mipango na mikakati ya kufikia malengo fulani katika maisha.Yawezekana mipango haiendi,changamoto zinakufanya ukate tamaa,umekuwa mtu wa kuhairisha, wewe muongeaji tu utendaji sifuri,ndoa na mahusiano ndio kikwazo cha wewe kutimiza ndoto zako?nini kikakwaz?” yanasema maelezo ya Dina.

“Tutakuwa na wazungumzaji na wahamasishaji,watu waliopitia changamoto za kimaisha lakini hawakukata tamaa wanaishi ndoto zao hivi sasa. Njoo tuzungumze,tubadilishane mawazo na tufurahi pamoja.Tutakuwa na band flani hivi kutuburudisha,” ameongeza.

Tukio hilo litafanyika November 8 kwenye ukumbi wa BNN uliopo Quality Centre jijini Dar es Salaam. Kila mshiriki atachangia shilingi 30,000 tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents