Burudani

Dogo watatu wafanya balaa Maisha Club

dogo_face
Katika wikiend hii, ukumbi wa New Maisha Club ulijukuta ukivamiwa na wingi wa watu hadi kushindwa kwa kuchezea baada ya kuwadondosha wadogo wa tatu wenye staili tofauti kabisa katika uimbaji kwenye muziki huu wa Bongo fleva.


Hapa nazungumzia Dogo Janja, Young D na Aslay ambao walikuwa gumzo na kusukumana na kuvutana kwa michano pale jukwaani ili kila mmoja amwangushe mwenzake. wapo wengine wakajisahau na kuwaita wadogo wenzake wazee, ilimradi kuleta mbwembwe. Ukumbini hapo watu walijaa kuliko kawaida, hadi mtu kutiririka jasho hata kama ulikuwa umekaa tu….

Dogo_aslay

Dogo_aslay2
Dogo Aslay alikuwa wa kwanza kupanda na kitu chake, ‘Naenda kusema’ kwakuwa alikuwa na show nyingine ndani ya Billcanas usiku huo huo katika uzinduzi wa video ya Chege na Temba ‘Kama ni Genstle au Sharobaro.
dogo_janja_2
Dogo Janja alifuata baadaye akaja kupigwa jeki na mtu mzima Tunda man kutoka makao makuu Tip Top
dogo_young_d
Young D, Young Rapa yeye akaja kufunga kazi kwa usiku huo, huku akiitroduce Single yake mpya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents