Burudani

Dr Cheni adai tasnia ya filamu Tanzania inakufa

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Dr Cheni amesema tasnia ya filamu inakufa kama uuzaji wa albamu za wasanii wa Bongo Flava ulivyokufa.

12141903_453867674798072_607685094_n

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Dr Cheni alisema kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali inazidi kuwa mbaya kwa wasanii wa filamu.

“Unajua kwa hali tuliyo nayo kwa sasa ni mbaya sana. Kama tukiendelea hivi na serikali ikashindwa kuchukua hatua mapema iwezekanavyo soko la filamu linakufa muda wowote,” alisema Cheni.

“Wasambazaji wanashindwa kuchukua mzigo mkubwa kutokana na piracy. Wasanii tupo wengi, kwahiyo kwangu mimi binafsi nina uwezo wa kutoa kazi nyingi kwa mwaka lakini kutokana na wasambazaji wetu pamoja na soko, unalizimika kutoa kazi moja au mbili na bado haulipwi vizuri, kutokana na piracy wanakuwa na kazi yako na wao wanauza mtaani. Mauzo ya albamu kwa wasanii yamekufa. Mimi naona kuna kila dalili ya soko la filamu kufa pia,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents