Burudani

Dudu Baya atoa baraka zote kwa TID kugombea ubunge

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Flava, Dudu Baya ameonyesha kuvutiwa na dhamira ya msanii mwenzie, TID kutaka kugombea kiti cha ubunge.

Dudu ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Dela Delani’ amesema anaamini kuwa TID anaweza kufanikisha hilo kwani eneo analotaka kugombea ni mzawa.

“Nilifurahi sana kusikia anataka kugombea ubunge  wa Kinondoni na ninaamini anaweza kwa sababu ni mzawa wa Kinondoni na anaijua vizuri ana influence ya kushawishi watu wampigie kura na mimi ningekuwa mmoja wapo ndoto yake ikatimia” amesema.

Tanzania ina wasanii wa muziki wawili ambao ni wabunge, Professor Jay na Sugu, Kenya kuna Jaguar na Uganda kuna  Bobi Wine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents