Michezo

Duka la London lakataa kumuuzia saa Samuel Eto’o sababu ni mtu mweusi!

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto’o amedai kuwa amewahi kuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi pindi alipoenda kufanya shopping kwenye duka moja jijini London.

Samuel Eto'o salutes Samdoria's fans at Genoa's Luigi Ferraris stadium after the draw with Palermo.

Mchezaji huyo raia wa Cameroon, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Italia, Sampdoria, ameiambia CNN kuwa alibaguliwa baada ya kwenda kununua saa yenye thamani ya £10,000.

Eto’o — ambaye kuna wakati aliwahi kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mshahara wa £350,000 kwa wiki, anasema alienda kwenye duka hilo akiwa na kaka yake lakini alitiliwa mashaka na muuzaji.

“Nilienda kununua saa kwenye duka, sio mbali na nyumba yangu. Saa niliyotaka kuiona ilikuwa ya gharama kubwa. Nilimuuliza muuzaji ambaye naye alikuwa mweusi, ‘unaweza kunionesha saa hiyo tafadhali?’
“Kwanza, nilimuona akigeuka kwa wafanyakazi wenzake kuuliza afanyeje. Hatimaye aliniacha niione saa. Niliiangalia na nikasema ‘sawa nitainunua’. Nilichukua credit card yangu na kwenda kuiweka kwenye mashine, alirudi na kusema kadi imekataliwa,” alisema.

Mshambuliaji huyo alimuuliza muuzaji huyo: Imegoma au ni wewe ndio hukutaka ikubali?” Aliendelea: Kaka yangu aliuliza, nini kinaendelea? Na muuzaji huyo akajibu ‘hapana hapana’. Ila kaka alisema ‘Hapana, kwasababu nilipoingia niliona jinsi nyote nyie mlivyokuwa mkituangalia. Kaka yangu anaweza kumudu hii na kwa jinsi mnavyomchukulia inaonesha jinsi mnavyodhani kwasababu ni mweusi, hawezi kumudu kununua saa hii.”

“Msichana huyo kisha alijibu: Hapana ni kwasababu tulipata wanaijeria hapa dukani siku iliyopita na walikuwa na credit cards feki.

“Sijui kama unaweza kuimagine uzito wa hicho alichokisema. Kama mwenzangu akifanya kosa wanatuhukumu sote. Sidhani kama ni mbaguzi wa rangi lakini alijumuisha watu wote weusi kama watu hao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents