Dume lenye Mimba

Unaweza kusema hii ni kali kati ya kali ambazo zimewahi kujiytokeza ulimwenguni, ambapo mwanaume aliyepata ujauzito hivi karibuni ameamua kujiweka hadharani kwa kuitangazia dunia kuhusiana na jinsi ameizoea hali yake hiyo

Dume lenye mimba


 


Unaweza kusema hii ni kali kati ya kali ambazo zimewahi kujiytokeza ulimwenguni, ambapo mwanaume aliyepata ujauzito hivi karibuni ameamua kujiweka hadharani kwa kuitangazia dunia kuhusiana na jinsi ameizoea hali yake hiyo ambayo kawadia inawahusu wanawake.


 


Kwa mujibu wa historia ya mkazi huyo wa Hawaii bwana Thomas Beatie kuwa alizaliwa akiwa ni mwanamke lakini hisia zake zilikuwa zikimpelekea ajihisi kuwa yeye ni mwanaume mpaka kufikia hatua ya kwenda kutoa matiti na kubadilisha nyeti zake na kuwekewa za kiume, pamoja na hayo aliamua kuacha uzazi kwani aliamini ipo siku atakuja kupata mtoto.


 


Kidume hicho kinachojulikana kwa jina la Thomas Beatie (34) alionekana katika kipindi cha luinga The Oprah Winfrey Show kinachoongozwa na mtangazaji maarufu duniani Oprah Winfrey huko marekani.


 


Dume lenye mimba akiwa na Oprah 
Thomas akiwa katika show ya Oprah


 


Mpaka sasa Thomas ana ujauzito wa miezi kadhaa baada ya kupandikizwa mbegu za kiume “Mimi ni binadamu kama wengine na nina haki ya kuwa na mtoto wa kuzaa wenyewe.”



“Ukweli kabisa nisingeweza kuyafikia maamuzi hayo endapo mke wangu angekuwa ana uwezo wa kushika ujauzito” alisema Thomas alipokuwa akifanya mahojiano na Oprah katika kipindi chake hicho huku kushoto mkewe anayejulikana kwa jina la Nancy ambaye aliondolewa kizazi.



Thomas alianza kwa kuondoa nywele zake za kifuani na kuanza kutumia madawa maalum kwa ajili ya kuongeza hormons za kike na kumfanya awe mwenye sua laini mithil ya mwanamke na baada ya maungo yake kukamilika na kuwa ya kike haswaa alipandikizwa mbegu za kiume.



Kijana huyu anatarajia kujipatia mtoto wa kiume siku za usoni ambao, “nataka kuwa na mtoto wa kumzaa mwenyewe vyovyote itwakayokua kwangu ni sawa tu awe wa kiume au wa kike.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents