Michezo

Everton yanasa saini ya Gylfi Sigurdsson

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Swansea City, Gylfi Sigurdsson mkataba wa miaka mitano kwa dau la pauni milioni 45 sawa na dola milioni 57.84.

Sigurdsson ambaye ameweka rekodi ya usajili katika kikosi hicho kinachonolewa na mdachi, Ronald Koeman anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya kikosi hiko hasa katika kipindi hiki cha msimu mpya wa Epl.

Meneja wa Everton, Ronald Koeman amesema kuwa kiungo mshambuliaji Gylfi Sigurdsson anakuja kuongeza makali ya kikosi hiko pindi tu atakapo malizana Swansea .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu ulipita aliisaidia Swansea kwa kuifungia mabao nane na kutoa pasi 13 zilizo saidia kupatikana kwa magoli.

Koeman amesema kuwa aliyekuwa mchezaji wao, Romelu Lukaku aliyeuzwa Manchester United mwezi uliopita kwa dau la paundi milioni 75 ni zao la Goodison Park hivyo anaamini mchezaji Sigurdsson amefanya chaguo sahihi la kwenda katika timu hiyo.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents