Michezo

Fahamu jinsi Kombe la ‘SportPesa Super Cup’ litakavyoendeshwa na ratiba yake ya msimu huu

Kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa baada ya kumalizana na Vilabu vitatu kwa udhamini wao sasa watangaza ujio wa Kombe lao (SportPesa Super Cup) ambalo litashirikisha timu 8 kutoka nchi mbili tofauti.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Bw Abbas Tarimba
Ligi hiyo itashirikisha timu nne kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza  Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11.
Utakuwa ni ushindani wa timu nne, kutoka Tanzania na Kenya, Hawa ni majirani na siku zote ni wapinzani wakubwa”, alisema Abbas Tarimba.
Kombe hilo litachukua Klabu nne kutoka Tanzania ambazo ni Yanga,Simba,Singida United na Jang`ombe boys huku Kenya ikiwakilishwa na Tusker fc,Nakuru All Star, Gor mahia na  FC Leopard zote kutoka Kenya.
Bingwa wa Kombe  la SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha Dola Elfu 30 sawa na Milioni 66 huku mshindi wa pili akipata Dola elfu 10 sawa na Shilingi Milioni 22 .
Kampuni ya SportPesa tayari wameidhamini Simba SC na Yanga SC kwa mkataba wa miaka mitano, huku wakimaliza usajili wao kwa Singida United ambayo imepanda daraja Ligi Kuu Bara msimu huu.
Ratiba ya michuano hiyo ya SportPesa Super Cup itakuwa kama ifuatavyo.
5/June/2017
Singida united Vs FC leopard
Yanga Vs Tusker fc
6/June/2017
Simba Vs Nakuru All Star
Jang`ombe boys vs Gor mahia
Nusu fainali itachezwa  tarehe 8 June huku Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker.
Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru all star atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor Mahia na fainali ya Kombe hilo itachezwa tarehe 11 June.
Tazama picha za hafla fupi wakati wa uzinduzi wa Kombe la SportPesa Super Cup.
Mkurugenzi mkuu wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba

Makamu wa Rais wa Simba Bwa Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyeshika tama.
Kocha wa Singida United ‘Hans van der Pluijm’ katikati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents