Michezo

Falcao ashindwa kurudi tena Atletico Madrid

Mshambuliaji wa Chelsea Radamel Falcao alikosa nafasi ya kurejea tena katika klabu ya Atletico Madrid siku ya mwisho ya usajili.

LONDON, ENGLAND - AUGUST 29: Radamel Falcao Garcia of Chelsea celebrates scoring his team's first goal during the Barclays Premier League match between Chelsea and Crystal Palace at Stamford Bridge on August 29, 2015 in London, England. (Photo by Paul Gilham/Getty Images)

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Colombia, ambaye kwasasa yuko Chelsea kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Monaco, alikuwa Uhispania usiku wa Jumatatu akiamini angerejea kwenye klabu hiyo ya La Liga.

Lakini matumaini yake yalikatizwa pale mchezaji Jackson Martinez, ambaye angeacha pengo Atletico, aliposhindwa kuhamia Uchina.

Hii ina maana kwamba hakukuwa na nafasi kwake kwenye klabu hiyo ya La Liga.

Falcao hadi sasa ameanza mechi moja pekee ya Ligi ya Premia akiwa Chelsea na bao pekee alilowafungia katika mechi 15 alizowachezea alilifunga baada ya kuingia kama nguvu mpya.

Mchezaji huyo mwenye miaka 29 alitua Stamford Bridge Julai mwaka jana baada ya kushindwa kufanya vizuri akiwa Manchester United kwa mkopo msimu wa 2014-15.

Hajachezea Chelsea tangu tarehe 31 Oktoba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents