MichezoUncategorized

Familia ya Sanchez yatua Uingereza

Familia ya Sanchez tayari washatua uingereza wakitokea kusini mwa marekani

Inafahamika kwamba, Manchester City walitaka kupata saini ya Sanchez lakini walishindwa kutoa dau la paundi millioni 60 wakati wa majira ya joto.Guardiola bado hajakata tamaa katika kumsajili nyota huyo wa Arsenal lakini atalazimika kuongeza dau ili aweze kunasa saini ya mchezaji huyo ambapo hapo awali City walitoa dau la pauni milioni 20 ambayo ni pauni milioni 10 nyuma ya dau walilotoa United.

Lakini wapinzani wao, Manchester United wanaonekana kupiga mbio za chini chini ili kumnasa mchezaji huyo wa Arsenal, kama vile walivyofanya Habari za hivi punde ni kwamba familia ya Alexis Sanchez wameshatua Uingereza kutoka Amerika ya Kusini.
na uhamisho wa Robin van Persie mwaka 2012.

Inasemekana kwamba timu ya Manchester United inataka kuwapa Arsenal kiasi cha pauni millioni 30 ili wamchukue Sanchez.United pia wapo tayari kumtoa Henrikh Mkhitaryan katika mpango wao wa kumnasa Sanchez.

Kama Sanchez atatua Old Trafford basi atalipwa kiasi cha pauni laki 4 kwa wiki na atakuwa ni mchezaji anaye pokea mkwanja mrefu zaidi katika ligi hiyo ya Uingereza
Liverpool nayo ni miongoni mwa timu inayotaka kunasa saini ya Sanchez toka walipo mpoteza Coutinho lakini timu hiyo haipo tayari kumlipa kiasi cha pauni laki 4 kwa wiki.

Mrithi wa Sanchez inasemekana kuwa ni Olivier Malcom ambaye kwa sasa yupo kwenye timu iitwayo Bordeaux ya ufaransa na Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 35 ili kumnasa straika huyo

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents